Kupitia mahojiano ya Episode aliyoyafanya David Letterman ya My Next Guest akiwa na Rapper Jay-z amefunguka kubwa kuhusiana na Kanye West na hii ni baada ya kuwamwagia sifa Eminem & Snoop Dogg
Kupitia mahojiano hayo Jay amefunguka kuhusiana na Kanye West na kubwa alilolisema ni kwamba kanye West Bado ni Kaka Yake tu.
Hov anasema,"Namuheshimu na ni kaka yangu japo hatujazaliwa na baba mmoja wala mama lakini nimekuwa nikimwangalia Kanye kabla hajawa na Album.Kitu ambacho kinafanya namheshimu ni mtu yule yule.Alikuwa anatuchanganya studio na anaanza kurap,na sisi tunakuwa kama tunamwambia ‘Could you please get down?’na yeye anasema hapana mimi ni mwokozi wa Chicago na alikuwa hana hata record moja."
EmoticonEmoticon