Rapper Lil Wayne amewaonya mashabiki zake kuhusiana na kutorusha chochote jukwaani wakati anaperfome huko Cannabis Cup ndani Sacramento weekend hii iliyopita.
Weezy alisopisha ngoma ya A Milli na kuwaambia mashabiki,"Kwa wote mtakaorusha chochote kwenye stage,sitajua kama ni upendo au mnajaribu ku promote kitu,lakini mimi natokea New Orleans na najua namna ya kukubaliana na upuuzi huo,na ninao watu wa New Orleans hapa na hao wanajua kurusha pia kurudisha kwenu kwa njia ya ku "Shoot"
Lil Wayne aliendelea kusisitiza na kusema kwamba hataki kuhusika na kifo cha mtu yeyote hapo.Hii sio mara ya kwanza kwa Rapper huyo kuwaonya watu wasirushe chochote kwenye stage ambapo yeye angechukua hatua endapo wangefanya hivyo.
EmoticonEmoticon