Msanii wa muziki kutoka nchini Uganda,(MOSES SSEKIBOGO) Radio amefariki dunia siku ya February 1 majira ya saa 12 asubuhi
Kwa mujibu wa mtandao wa New Vision umeripoti kwamba Manager wao Balaam Barugahara ambaye wameongea naye kwenye simu na kuwaeleza kuwa Radio amefariki Leo asubuhi majira ya saa 12, na wanajiandaa kuupeleka mwili wake katika hospitali ya Mulago.
Msanii huyo ambaye alikuwa akifanya vizuri na mwenzie Weasel, tangu January 23 mwaka huu hali yake ilikuwa ikiripotiwa kuwa mbaya kufuatia majereha aliyoyapata kutokana na ugomvi wa klabu.
Hapo jana Rais wa Uganda, Yoweri Museven alitoa Milioni 30 kwa ajili ya matibabu ya msanii huyo, pia kulikuwa na maombi maalumu yalikuwa yameandaliwa kwa ajili ya kumuombea ambayo yalitarajiwa kufanyika February 4 mwaka huu katika kanisa la Light the World.
Mwanamuziki Radio Jina lake kamili ni Mosses SSekibogo na amezaliwa mwaka 1985 nchini Uganda na amefariki akiwa na umri wa miaka 33.
Baadhi ya ngoma ambazo alishawahi kufanya powa ni pamoja na Heart Attack, Sweet Lady Can't Let You Go, pamoja na Zuwena
R.I.P
EmoticonEmoticon