Msanii wa muziki kutoka Canada, The Weeknd amewaonya wasanii wa muziki dunia akiwemo Wizkid kuacha mara moja kutumia neno ‘StarBoy’ kwa madai kuwa neno hilo ameshalilipia (TradeMark) kwa matumizi yake ya kibiashara.
The Weekend amesema kuwa yeye ndiye muanzilishi wa neno(nembo) hiyo ya ‘StarBoy’ na yeyote atakayetumia atachukuliwa hatua za kisheria.
Kwa mujibu wa mtandao wa TMZ, Tayari wanasheria wa The Weeknd wameshaandaa nyaraka za kuwaburuza Eymun Talasazan mahakamani kwa kutumia nembo hiyo kwenye vipindi vyake vya TV baada ya The Weeknd kuachia album yake ya ‘StarBoy’ mwaka 2016.
Eymun Talasazan ilitaka kusajili kipindi cha Tv cha Starboy siku 11 baada ya studio za MARVEL kuthibitisha ujio wa kitabu cha vikatuni cha Starboy kitakachomuhusisha The Weeknd, kitabu hichi kinatoka June 2018.
EmoticonEmoticon