Rapper Eminem amepongezwa na Recording Industry Association of America (RIAA) kuwa msanii aliyeuza zaidi ya kopi milioni 100(Diamond certification) za nyimbo zake 3.
RIAA Wametangaza rekodi hii baada ya wimbo wa “Lose Yourself” kufikia kopi Milioni 10(Diamond Certification), huku colabo yake na Rihanna “Love the Way You Lie” ikiwa na mauzo ya kopi Milioni 12(Diamond certification) na “Not Afraid” 10 Million (Diamond certification).
Kupitia account yao ya Twitter RIAA wameandika,"Congratulations to @Eminem! 107.5 million song awards. Three Diamond Songs. #RIAATopCertified http://bit.ly/RIAATopDigital"
Eminem sasa ameuza kopi Milioni 107.5 na kuvunja rekodi ya Taylor Swift ya kopi Milioni 106.5 huku Rihanna akiongoza kwa kuwa na mauzo ya kopi za nyimbo Milioni 121.Congratulations to @Eminem! 107.5 million song awards. Three Diamond Songs. #RIAATopCertified https://t.co/sXt0Fz6Ke9 pic.twitter.com/Df9rxfC1BS— RIAA (@RIAA) February 28, 2018
EmoticonEmoticon