TUMIA BIDHAA BORA ZA AZAM BAKHRESA

Ujumbe Wa Diamond Platnumz Baada Ya Kusikia ALIKIBA Ameoa,"Nimeambiwa King Kiba kaoa leo..."

Leo April 19, 2018 msanii Alikiba ameoa, mshindani wake kimuziki Diamond Platnumz hajakaa kimya kwenye hilo.

Diamond amefunguka kuwa amepewa taarifa za Alikiba kuoa siku ya leo, hivyo amemtumia salamu na kumtakia maisha mema ya ndoa. Kupitia ukurasa wake wa Intagram Diamond Alichokiandika,"Wadau Nimeambiwa King Kiba kaoa leo...Mfikishieni Salam zangu, za Ndoa njema, na Maisha yenye Furaha, Amani na Baraka tele...🔥🔥🔥"



Msanii Alikiba amefunga ndoa na mpenzi wake  Aminah Rekish asubuhi ya leo mjini Mombasa nchini Kenya. Pia Utakumbuka Diamond alishaweka wazi mipango yake ya kuoa mwaka huu. 


EmoticonEmoticon