TUMIA BIDHAA BORA ZA AZAM BAKHRESA

Mipango Ya Diamond Platnumz Ni Kufunga Ndoa Mwaka Huu,Mama Yake Amekuwa Akimpigia Kelele Kuhusiana Na Hilo

Msanii Diamond Platnumz Finally anataka kuondoka katika group la Ukapela na kuweka chombo ndani ambapo swala la kuoa limekuwa ni kilio kikubwa toka kwa mama yake kumtaka kuwa afanye hivyo.

Diamond amefunguka swala lake la mipango ya ndoa kwa mwaka huu kupitia account yake ya instagram wakati akiwa anamtakia mama yake Happy Women's day,na kufunguka kwamba jambo hilo la kuoa limekuwa likitakwa sana na mama yake mzazi.

Diamond ameandika,"Happy Women's day Mama na wanawake wote Ulimwenguni... Nashkuru sana kwa kunizaa na kunilea...Wewe ni Mboni na Nguzo ya Maisha yangu mama...Licha ya shida na Mateso uliyoyapata kwenye kunizaa na kunilea, lakini hata sasa ambapo ulitakiwa walau Upumzike nimekuwa nikikukosea kwa kukuingiza hata kwenye Matatizo Yasiyokuhusu...Wanakutukana, wanakukebehi na kukutupia kila neno lililo baya, yote kwa sababu yangu mimi, lakini sikuzote umekuwa mwenye kunisamehe, kunipenda na Kunithamini.....Nakupenda sana Mama, Na nisameh kwa yote nilokukosea... Inshaalah, Mwenyez Mungu anibariki Mwaka huu Mwanao nifanikishe Ndoa yangu na kukupa Furaha ya Milele ambayo siku zote umekuwa Ukiitaka..... @mama_dangote" 

Few Days a go Diamond Platnumz aliachana na Zari bt kumeonekana kwamba bado anampenda Zari.

Let's Wait & See.Keep In-Touch 

 


EmoticonEmoticon