Kitendo cha Diamond Platnumz kuonekana na Wema Sepetu Last Night
kimeibua mengi hasa kwa mashabiki pamoja na watu mbali mbali kuhusiana na wao kukumbatiana na Wema kumkaribisha Jukwaani.Kupitia account ya Diamond Platnumz ya Instagram amwaga povu kwa mashabiki ambao hawakupenda kumwona yeye pamoja na Wema, kwa kuweka video wema akimkaribisha jukwaani na caption inayosema,
"Wengi Hupenda kuona watu wakiwa wana Vita ama uhasimu usio na kichwa wala miguu... Eti utamsikia mtu anasema "Dogo Mi shabiki yako Mkubwa na nakukubali sana ila kitendo cha kumualika Wema Umeniuzi" kwaio we unataka mie niendelee kuwa na vita ama niwe na vita na Wema ili iweje? yani mie nikiwa na vita na Wema we unafaidika nini? na itanisaidia ama kusaidia nini kwenye Sanaa yetu? Huwezi kuwa shabiki yangu halaf unafurahia mie kuendelea kuwa na vita na mtu, tena vita ambayo imeshaisha...nina familia yangu Naipenda Naiheshimu na siwezi kuiacha... ila hio sio sababu ya kuwa na vita na watu...na huu ni mfano wa kwanza mwingine unafata.... Huu sio Muda wa kujenga chuki zisizo za msingi ni wakati wa wasanii kushirikiana na kwa pamoja kufanya kazi na kukuza sanaa zetu kwajili ya future ya wadogo na vizazi vyetu vijavyo... Shukran sana Mdam kwakuja usiku wa jana...Mwenyez Mungu akubariki na akujalie kila la kheri uliombalo..... #Watakubali by @Mbosso_ link in his and my BIO"
EmoticonEmoticon