TUMIA BIDHAA BORA ZA AZAM BAKHRESA

Maswali 5 Ya Kuyajua Aliyoyajibu Kendrick Lamar Aki Cover Jarida La Rollingstone

Rapper Kendrick Lamar ame cover Jarida la Rollingstone na ameweza kufunguka mengi kuhusiana na Jay-Z,Nyimbo zake bora kwa Drake na ushauri.,kuhusiana na Rapper Future,ghostwriters(waandikiwaji wa nyimbo),Wack artist na mengine mengi.

1:Kwenye ngoma ya ELEMENT kuna mambo 2 yamehusishwa humo ndani kati ya Black artist & Wack artist.Maana na Wack Artist ni nini?
Kendrick Alijibu"Ni msanii anayetumia muziki wa mtu mwingine kwa idhini yao,naonglea mtu ambaye anaogopa kufanya muziki kwa sauti yake ya kipekee,mtu anayefwata mafanikio ya mtu fulani na mambo yake huku yeye akisahau kuwa anaacha mambo yake.Na hilo ndyo linafanya game hii ya muziki iwe chini.Kila mtu hawezi kuwa Kendrick Lamar.Na siwaambi mrap kama mimi,Be You,Simpe As That"

2:Kuhusiana na Rapper Future kwasababu pia wameshafanya ngoma ya pamoja kama Mask Off Remix?
Kendrick Alijibu,"Ni genius wa kipekee,nimemwangalia studio kwa jinsi anavyoitikia melody(huku anasnap kidole)kama hivi,nadhani anakuwa katika maadhi fulani ya ki R&B na ana akili kubwa sana ya kuusoma muziki kama mimi nliyonayo."

3:Ngoma Ya Drake anayoipenda sana?
Kendrick Alijibu,"Nina ngoma nyingi sana ambazo Drake amefanya ninazikubali,anazo nyingi sana"
(USHAURI KWA DRAKE AIMBE AU A RAP?)
Kendrick Lamara alijibu,"Afanye Vyote"

4:Katika Mixtape ya kipindi cha Nyuma ya Kendrick akiwa na miaka 16 alikuwa ana sound kama Jay-Z,Lipo vipi Hilo?
Kendrick Alijibu,"Oh Yeah That's my guy,still is.mimi bado ni shabiki na ile ni kama page ya kitabu nliyochukua toka kwake,kuwa na uwezo wa kuchukua mashairi kwenda kwenye maongezi na kufanya kama nimekaa hapa na naongea na wewe."
(STYLE YAKE YA KUIMBA ULIIPATAJE?)
Kendrick Alijibu,"Nadhani ni siku nliyosema nitakwenda kununua my real name,Kendrick Lamar na baada ya kufanya hivyo ilikuwa rahisi kwangu kutafuta sauti yangu kwasababu hakuna mtu atakayekuelezea story yangu kama mimi ninavyokuelezea"

5:Ni sawa kwa Rapper Kuandikiwa(Ghostwriter),cs wewe pia ulishamwandikia Dr Dre?
Kendrick Alijibu,"Inategemea na uwanja unaojiingiza,Najiita mwenyewe best Rapper na siwezi kujiita best rapper kama naandikiwa.Kama wewe unasema ni msanii wa tofauti na haujali kuhusiana na kanuni zozote za kuwa best rapper,then so be it,fanya muziki mzuri bt jina halitokuwepo"



EmoticonEmoticon