Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Harisson Mwakyembe leo Machi29, 2018 ametangaza kufuta adhabu ya kufungiwa kwa msanii wa muziki Roma Mkatoliki.
Akizungumza na Waandishi wa Habari katika Ofisi ya Wizara hiyo jijini Dar es salaam Waziri Mwakyembe amesema kuwa muda wowote kuanzia sasa Roma Mkatoliki atakuwa huru kufanya shughuli zake za muziki kama ilivyokuwa awali kwa sharti moja la kukamilisha taratibu za kujisajili BASATA.
Roma ambaye naye aliongozana na Waziri Mwakyembe amesema kuwa hata kama ameachiwa huru lakini wimbo wake wa kibamia ameviomba vituo vya redio na runinga kutocheza wimbo huo baada ya kufutiwa adhabu yake.
EmoticonEmoticon