TUMIA BIDHAA BORA ZA AZAM BAKHRESA

Roma Afungiwa Kufanya Muziki Na Ngoma Zake Kutokupigwa Redioni & Tv (VIDEO)

Serikali kupitia Wizara ya Habari, Sanaa na Utamaduni imemfungia kifungo cha miezi sita msanii wa muziki wa Hip Hop nchini Tanzania, Roma Mkatoliki kutojihusisha na shughuli zozote za muziki baada ya kukaidi agizo la kubadilisha wimbo wake wa Kibamia.

Akitoa adhabu hiyo, Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Juliana Shonza amesema kuwa Roma amedharau wito wa serikali ambapo leo aliitwa ili ahojiwe  kutokana na wimbo wake huo ikiwa ni hatua ya pili mara baada ya Baraza la Sanaa Nchini Basata kumuita na kumtaka arekebishe baadhi ya sehemu katika wimbo huo.
Mhe. Shonza amesema kuwa adhabu hiyo itajumuisha na nyimbo zake zote kutokupigwa Redioni wala kwenye runinga kwa muda wote aliyofungiwa.
Kwa upande mwingine, Mhe. Shonza amesema Serikali itaangalia mwenendo wa msanii wa Bongo Fleva, Nay wa Mitego ambaye naye aliitwa na kukiri makosa na kuahidi kubadilika.

This article Original appeared in BONGO 5


 SOMA NAY WAMITEGO KUACHA MUZIKI


EmoticonEmoticon