TUMIA BIDHAA BORA ZA AZAM BAKHRESA

Live Imethibitishwa Cardi B Ana Ujauzito Na Muda Wa Kujifungua

Hatua inakuja baada ya Cardi B na Offset kukataa maneno yaliyokuwa yanaendelea na kusema kwamba Cardi ana ujauzito wa Offset.

Mtu wa karibu na Cardi B ameieleza TMZ mpaka mwanzoni mwa mwezi wa Saba July,Cardi B atakuwa karibuni kujifungua na Report zinasema kwamba akiwa na mimba ya miezi 7 Cardi ata perform katika tuzo za Coachella April.

Katika tuzo za Iheart Radio Cardi B alivaa nguo ambayo ilificha ujauzito huo na watu kutokuwa na uhakika juu ya hilo wakati alipopanda stage kupokea tuzo na wakati wa Performance
Imeelezwa pia Cardi B hatoachia mpunga wa show kubwa ya Tour ya Bruno Mars ambayo itamwingizia Dola $100,000( Million 226,115,000 TSH) kwa usiku mmoja September,ambapo atakuwa ametoka kujifungua miezi miwili tu iliyopita.


Mwezi uliopita kwa upande wa Offset alikataa kuhusiana na swala hilo la ujauzito wa Cardi B na kusema,"Mimi ni baba wa watoto 3 tu,Watoto wangu wana miaka 2, 2, na mkubwa ana miaka 8,Sina uwezekano mwingine."

Kwa upande wa Cardi B alikataa taarifa za ujauzito wake kwa aliandika,No bitch I’m just getting fat. Let me fat in peace(Hapana nina nenepa,acheni ni nenepe kwa amani).”




    


EmoticonEmoticon