TUMIA BIDHAA BORA ZA AZAM BAKHRESA

Taylor Swift Avunja Record Ya Mauzo Ya Mwaka Kwa Album Yake.

Mwanadada Taylor Swift amefanikiwa kuvunja record na Album yake iliyotoka Nov 10 ya Reputation na kuipiku record iliyokuwa imewekwa na Ed Sheeran ya mauzo ya Album yake ya Divided kwa mwaka 2017

Kwa mujibu wa Nielsen Music wameripoti kwamba Album ya Reputation ya Taylor imeweza kuuza Copies 1.05 million ndani ya US kwa siku nne za kwanza album ilipoingia sokoni.

Imekuwa ni Album ya pili kuuza copy Million ndani ya week moja ambapo ya kwanza ilikuwa ni 25 ya Adele ambaye aliuza copies 1.16 Million kwa week ya kwanza ilipoingia sokoni mwaka 2015

Kwa mwaka 2017 Taylor Swift amempiku Ed Sheeran ambaye alikuwa ameshikilia record kwa kuuza copies 919,000 na Album yake ya Divided kwa week ya kwanza.

Reputation Right now ndyo album iliyo na mauzo makubwa kwa mwaka 2017 ndani ya US pekee na inategemewa kuingia katika chart za Billboard no1 katika week inayokuja.Keep In-Touch


EmoticonEmoticon