TUMIA BIDHAA BORA ZA AZAM BAKHRESA

Ariana Grande Yupo Tayari Kuiachia Album Yake Mwaka Huu.Ametangaza Jina Na Tarehe (VIDEO)

Ngoma ya kwanza kwa mwaka 2018 No Tears Left To Cry imeonyesha mwanga mzuri na mwanzo wa mafanikio kwa album mpya ijayo ya Ariana Grande baada ya kukamata nafasi ya 3 Billboard Hot 100 kwa week ya kwanza.

Ariana pia amekaa chini na Jimmy Fallon kwenye Tonight show na kuongelea album yake jina na tarehe kamili ya kutoka.

Ariana anasema,"Albamu yangu inakuja msimu huu,nimefanya kazi na Pharrell, Max [Martin], Ilya, na Savan [Kotecha].Inaitwa Sweetener  kwa sababu ni aina ya kuleta mwanga kwa hali au maisha ya mtu au mtu mwingine ambaye huleta mwanga kwa maisha yako au kupendeza hali."

Aliweza pia kutumia account yake ya Twitter kuwajuza mashabiki kwa kuandika jina la album kwa herufi zilizogeuka juu chini.
Album ya Sweetener inategemewa kuingia sokoni July 20 mwaka huu na hiyo iligundulika baada ya Ariana kusema katika Interview,"Mimi nitafanya kitu maalum kila tarehe 20 na kuna tarehe 20 tatu tu mpaka jambo hilo kubwa."


EmoticonEmoticon