TUMIA BIDHAA BORA ZA AZAM BAKHRESA

Bungeni,"Diamond Platnumz Achongewe Sanamu"...Basata,Kosota Wapigaji Wa Hela Za Wasanii (VIDEO)

Msanii Diamond Platnumz kutokana na mafanikio makubwa yanayoletwa na jitihada zake,ametokea kutupiwa sifa kubwa bungeni mpaka kufikia hatua ya kutaka achongewe sanamu kwa juhudi zake.


Godluck Mlinga Mbunge wa Ulanga amefunguka bungeni na kusema,"Naomba nikupongeze Diamond popote ulipo Ingekuwa amri yangu,tungechonga sanamu la Diamond tukaliweka pale kwenye ule mnara wa askari,ule mnara tumeuchoka,ametufikisha mbali,ni alama.ameitangaza nchi yetu huko mbele."


Lakini pia Mbunge huyo pia alifunguka swala la kusaidia wanamziki na kusema kwamba wanamziki wanapenya wenyewe wenyewe, huku wakikutana nao mbele wanajifanya wamewasaidia."Tumeweka vyombo vya kuwatapeli....sijui kuna Basata,Sijui kuna Kosota,hawa ni wapigaji wa hela za wasanii,hamna lolote wanalolifanya."Aliongea Mbunge huyo.

Fulll Video ya Aliyoyaongea Au Audio zipo hapo chini  


AU SIKILIZA AUDIO


EmoticonEmoticon