TUMIA BIDHAA BORA ZA AZAM BAKHRESA

Ed Sheeran Amefunguka Mambo 4 Muhimu Katika Interview Ya Ellen Show (VIDEO)

Hit Maker wa Divide amefanikiwa kukaa chini kwenye show ya Ellen Degeneres na kufunguka mambo mengi ikiwemo Album na Nyimbo yake ya Shape Of You kutokupata nafasi katika Tuzo za Grammy 2018 kwenye category ya Album Na Best Song,kuhusiana na Remix ya Perfect na Beyonce,ngoma anayoipenda kwenye last Album yake na mengine mengi.

Kuhusiana na ngoma yake Shape Of You na Album kutopata nafasi katika tuzo za Grammy 2018 kwenye kipengele cha Best Album na Best Song,alifunguka na kusema

"Ninavyoona baadhi ya mwaka unao mwaka wako na baadhi ya mwaka pia unaweza usiwe mwaka wako,na maybe mwaka huu sio mwaka wangu"

Kuhusiana na wimbo anaoupenda katika Album yake ya Divide Alisema ni Perfect na Aliweza kueleza sababu za kuupenda wimbo huo,

"Kwasababu ni moja kati ya wimbo nlioandika kwa haraka sana na ni wimbo ambao nliandika wa kwanza katika Album na nlikuwa nausikiliza na kuendelea kuupenda"
Aliongelea kuhusiana na Perfect Remix ambayo amemshirikisha Beyonce ambayo ilitoka December 1 na aliweza kufunguka alimpataje Beyonce,

"Wazo lilinijia mwanzo na nikataka niifanye peke yangu bt nikawaza nikasema,nampenda Beyonce,"ntamwambia Beyonce"huku kwenye kichwa changu najua Beyonce atasema no,na nikawa well inabidi nimfwate nimuulize kwanza,nikaenda na akaniambia powa."

Kuhusiana na Mahusiano yake na mpenzi wake Right now anasema,

"Nimekuwa na mahusiano na mpenzi wangu kama kwa miaka 3 na tumemaliza naye high School,yuko powa na tunaishi pamoja."

FULL STORY KWA NJIA YA VIDEO


EmoticonEmoticon