TUMIA BIDHAA BORA ZA AZAM BAKHRESA

Wizkid Amefunguka Maswali 5 Muhimu Ya Kuyajua Kupitia Apple Music Beats One Radio

Msanii toka Nigeria Wizkid baada ya kuachia Mixtape yake ya Sound From The Other Side na kufanya vizuri,Right now Wizkid amefunguka mengi.

Kupitia Apple Music Beats One Radio Wizkid alikuwa anafanyiwa mahojiano na Ebro na kufunguka kuhusiana na Mixtape yake,kwanini asingeifanya Album,Mahusiano Yake na Ty Dolla $ign na kunaweza kukaja Album ya pamoja,Title ya Ngoma Yake na TreySongz, Wasanii anaowakubali Africa,producers na watu anaotamani kufanya nao collabo na mengine mengi.
Maswali 5 Muhimu unayotakiwa kuyajua Wizkid Aliyoyajibu.

1:Kwanini Asingeifanya Mixtape Ya (SFTOSD) kuwa Album cs ime contain ngoma kali na Collaboration kali?

Wizkid alijibu, “Kila mtu anaiita hii ni Album bt mimi naiita Ep,na wakati nlivyokuwa naitengeneza project hii nlikuwa nataka niifanye na watu waipate bure bt rafki yangu alikuja na kuniambia unaachia kazoo hii halafu unataka watu waipate bure?Hell No!!!!

Kwa kawaida Mixtape haziuzwagi huwa zinatolewa Free kwa kuwekwa kwenye platform kama Audiomack,Soundcloud na kwingineko ili watu wa download free bt ya Wizkid imewekwa Itune ili watu waweze kununua cs alishauriwa ina ngoma kali.That’s Why mzigo unauzwa Itune.

2:Mahusiano Yake Na Ty Dolla $ign na Wanategemea kufanya Album pamoja?

Wizkid Alijibu, “Tulikutana London na ni mmoja kati ya watu wenye vipaji sana na tulikaa studio kwa lisaa 1 na tukawa pamoja tukafanya ngoma kibao,bt hauwezi jua kama tutaleta collabo ya album na vitu vingine.”

Ngoma waliyofanya pamoja na ina Hit right now na hautochoka kuisikiliza ni Dirty Wine,Imefanywa na Dj Mustard, na inapatikana katika Mixtape hiyo.

SIKILIZA AUDIO HAPA


3:Title ya ngoma aliyoifanya na Trey Songz ambayo ni moja kati ya ngoma kali pia.?

Wizkid alijibu, “Ngoma inaitwa Bese na inamaanisha,kwasababu yaw ewe mschana mimi ntakwenda kudaiwa au kupata madeni kwa kupoteza pesa zangu.”


Moja kati ya Club Banger ni pamoja na ngoma waliyofanya na Trey Songz inaitwa GBese inayopatikana katika mixtape hiyo.

SIKILIZA AUDIO HAPA

4:Baadhi ya wasanii anaowakubali Africa?

Wizkid alijibu, “Burna Boy,Mr Eazy,Wande Coal na 2face(2baba)."

5:Ma Producer anaotamani kufanya nao kazi na hana connection nao na pia anaowakubali katika Collabo?

Wizkid Alijibu, “Pharel Williams,Kanye West,Damian Marley ambaye nina ndoto naye kubwa ya kufanya naye kazi na kila moja nliyefanya naye collaboration nilikuwa na ndoto naye kubwa ya kufanya kazi."

TAZAMA FULL INTERVIEW HAPA


EmoticonEmoticon