TUMIA BIDHAA BORA ZA AZAM BAKHRESA

Kanye West Ajiondoa TIDAL YA Jay - Z


Rapper Kanye West amejitoa kwenye mtandao waTIDAL wa Jay-Z kisa kikitajwa kuwa ni maslahi ya kifedha.


Kwa mujibu wa TMZ, Kanye alikuwa kiungo muhimu ndani ya mtandao huo wa kutazama na kusikiliza kazi za muziki, TIDAL ilipata wateja wengi zaidi baada ya album ya Kanye West SAINT PABLO kutoka kupita mtandao huo.
Sababu za kujitoa zimetajwa kuwa ni kushindwa kuelewana kwenye masuala ya malipo na kampuni ya TIDAL na maneno makali ya Jay Z kwa Kanye Westkwenye album yake mpya ya 4:44.
Wanasheria wa pande zote mbili wanajipanga kwenda mahakamani. Inasemekana Kanye amekuwa akilalamika kuwa anawadai TIDAL dola milioni 3.


EmoticonEmoticon