TUMIA BIDHAA BORA ZA AZAM BAKHRESA

Justin Bieber Amgonga Paparazi Na Gari Yake

Msanii Justin Bieber amejikuta akiingia katika matatizo baada ya kumgonga moja kati ya mapaparazi kwenye mguu aliyekuwa anataka story kutoka kwake na gari aina ya Pickup  baada ya Justin kuripotiwa kuwa alikuwa ametoka kanisani.

Alichokisema Justin baada kumgonga mpiga picha huyo na kutoka kwenye gari ni,"Nyie watu mlikuwa wote mbele ya gari na ilikuwa ngumu...,na mnanihofia kuhusu mimi au huyu hapa chini?Nyie watu mnafanya nini?Huyu mtu yupo hapa chini na nyie mnaniuliza kuhusu mambo yenu,wekeni Camera chini na mtoe msaada."

Justin aliendelea kusema,"Nlikuwa sioni kitu kwasababu nyie mlikuwa mnanipiga picha",bt aliendelea kumwambia aliyeumia kwamba,"nataka kuhakikisha kwamba upo sawa hapo na kama kuna kitu chochote unahitaji nikusaidie niambie".

Bieber alikaa pale kwa muda mpaka watoa huduma ya kwanza wapokuja na polisi pia.

Kwa mujibu wa Taarifa za polisi zinasema kwamba Bieber alikuwa katika mwendo mdogo sana.

Kupitia mtandao wa kijamii wa paparazi huyo aliandika kwamba,"Nipo salama,He is a good kid na nadhani truck ile ilikuwa kubwa sana kwake so ilikuwa ngumu sana kuona mbele,ajali zinatokea na kila kitu kipo salama hapa".

Tazama video hapo chini Tukio zima. 


EmoticonEmoticon