TUMIA BIDHAA BORA ZA AZAM BAKHRESA

Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Spotrs. Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Spotrs. Onyesha machapisho yote

WEKA NYIMBO YAKO KWENYE GOOGLE/INTERNET HAPA.

  1. Tuma Cover Pamoja na Nyimbo(Official Audio)kupitia sehemu zifuata;


  • Email:thedruidboy@gmail.com(hakikisha email ni herufi zote ni ndogo hata ya kwanza)
  • Whatsapp:0714-489394
      2. Gharama za kuweka nyimbo kwenye Internet(mtandaoni)kupitia Site ya Mullastar;
  • AUDIO: Tsh 20,000 Nyimbo 1/Kwa Album Tsh 10,000 Nyimbo Kwa wimbo 1.

     2. Endapo utahitaji nyimbo yako iweze kuuzwa pia kupitia Mullastar,Jambo hilo litawezekana endapo nyimbo yako itakuwa katika Platform za Tanzania za kuuzia muziki ambazo ni, WASAFI.COM pamoja na MKITO.COM

NOTE:Malalamishi yoyote yatakayowasilishwa kuhusiana na nyimbo ambayo sio haki ya mtu aliyeiwakilisha,Itafutwa ndani ya masaa 24 kama aliyeiwakilisha hatojibu malalamishi.

Kwa Maelezo zaidi Piga.0714-489394.

Ronaldinho Bye Bye (Kwaheri)

Nyota wa zamani wa timu ya taifa ya Brazil na klabu za PSG, Barcelona na Ac Milan Ronaldo de Assis Moreira Maarufu kama Ronadinho Gaucho amestaafu soka.

Licha ya Ronadinho kutocheza soka la kiushindani toka mwaka 2015 amekuwa akicheza michezo ya mabonanza
Kaka na wakala wa mchezaji huyo Roberto Assis amethibitisha kuwa umefika mwisho kwa fundi huyo wa Brazil kucheza soka.
Ronaldinho alianzia soka yake katika klabu ya Gremio ya nchini kwao kabla ya kujiunga na Paris St-Germain mwaka 2001 na baadaye kujiunga na Barcelona alikong'ara sana.
Katika msimu wa 2010 -2011 alijiunga na AC Milan ya Italia kabla ya kurudi kwao na kujiunga na Flamengo mwaka 2011. Kisha alichezea vilabu vya Atletico Mineiro, na Queretaro ya nchini Mexico na kurudi tena kwao Brazil katika klabu ya Fluminense.

Tetesi za soka Ulaya Julai 15

Meneja wa Arsenal, Arsene Wenger amekuwa akimtumia ujumbe mfupi wa maandishi Alexis Sanchez, 28, kujaribu kumshawishi asiondoke Emirates.
Mshambuliaji wa Monaco Kylian Mbappe ameonesha dalili za kuondoka katika klabu yake hiyo huku Arsenal wakiendelea kumnyatia.
Chelsea wana uhakika wa kuwapiku Liverpool katika kumsajili Pierre Emerick-Aubameyang, 28, kutoka Borussia Dortmund, ambao sasa wameanza mazungumzo ya kumtaka Olivier Giroud wa Arsenal.
Nemanja Matic, 28, huenda akajiunga na Juventus baada ya Chelsea kumruhusu kutojiunga na kikosi kinachokwenda China na Singapore kwa ajili ya mechi za kujiandaa na msimu mpya. Diego Costa pia ameachwa.
Arsenal wameonesha dalili za kumtaka Nemanja Matic, na wapo tayari kubadilishana na Alex Oxlade-Chamberlain, 23.
Kasper Schmeichel, 30, amepata matumaini ya kujiunga na Manchester United baada ya taarifa kuwa Real Madrid wamepanda dau la kumtaka David de Gea, 26.
Manchester United wana uhakika Real Madrid hawataiweza bei ya David de Gea.
Iwapo David de Gea atakwenda Real Madrid, meneja wa Manchester United atataka mchezaji mmoja kutoka Real Madrid na huenda akamtaka beki Rafael Varane.
Kipa namba tatu wa Manchester United, Joel Pereira, 21, ana nafasi ya kuwa namba moja iwapo De Gea ataondoka.
Inter Milan huenda wakamuulizia mshambuliaji wa Manchester United Anthony Martial wamchukue kwa mkopo kama sehemu ya mkataba wa United kumsajili Ivan Perisic, 28.
Tottenham watachuana na Juventus katika kumsajili beki wa Porto Ricardo Pereira, na watatazamiwa kulipa pauni milioni 22, kumchukua mchezaji huyo kuziba pengo la Kyle Walker.
Joe Hart anakaribia kukamilisha usajili wake wa pauni milioni 10 kutoka Manchester City kwenda West Ham.
Meneja wa Manchester United Jose Mourinho hatoishutumu bodi ya klabu kwa kushindwa kumsajili Alvaro Morata.
Liverpool huenda wakapanda dau la pauni milioni 65 kutaka kumsajili kiungo wa RB Leipzig Naby Keita, 22.
Roma wanajiandaa kupanda dau la pauni milioni 30 kumtaka winga wa Leicester Riyad Mahrez, 26.
Meneja wa Birmingham Harry Redknapp anataka kumsajili beki wa zamani wa Arsenal na Chelsea, Ashley Cole, 36, kutoka LA Galaxy.